Wednesday, July 8, 2009

WAZEE WA URODA WAAMBULIA NGOMA KWA SAIDA KAROLI


SAIDA KAROLI ambaye aliwai kutamba na kibao cha chenkula, chambua kama karanga na vibao vingine vikali alivofanya kiasili ya bukoba vilivyomuweka juu siku za nyuma karibuni na kufanya nyota yake kukua Tanzania nzima.
Mwanadada huyo mwenye asili ya kihaya hivi karibuni alipata kufanya show nyumbani hapo bukoba show ambayo ilikua ikisubiriwa na wengi mkoani hapo.Mwanablog wetu alifanya uchunguzi ali kuweza kubaini ni kwa nini watu walikuwa wakisubiri kwa hamu show ya mwanadada huyo ambayo ilisindikizwa na wasanii wakali wa bongo kama Hardmad, chidi benz na berry 9 ambaye anatamba sasa na kibao cha SUMU YAPENZI.
uchunguzi wa mwanablog wetu ulionyesha kwamba wengi walimsubili mwanadada huyo kwa sababu siku nyingi zilipita bila ya kusikika hewani mwanadada huyo lakini tathmini nyingine ilionyesha kuwa wazee wengine majina yao yanaweka kapuni walikwenda kwenye show ya saida karoli kwa ajili ya kumsalandia lakini juhudi zao ziligonga mwamba,walijikuta wakiishia wakicheza ngoma kwenye show bab kubwa aliyopigwa na mwanadada huyo

1 comment:

  1. Niby Internet jest pełen przeróżnych artykułów, jednak nieczęsto udaje mi się natknąć na coś tak krótkiego, jak ten wpis. Muszę oznajmić, że niezwykle fajny wpis… miło mi się go czytało i okazał się niebywale pomocny.

    ReplyDelete